Adidas yasitisha kufanya kazi na Kanye West

Adidas yasitisha kufanya kazi na Kanye West

Ooooooh! Waswahili wanamsemo wao bwana salimia watu pesa huishaa, basi bwana gumzo mitandaoni week hii ni kuhusiana na sakata kubwa la rapa Kanye west kufirisika baada ya mkataba wake kuvunjwa na kampuni ya Adidas.

Kampuni hiyo kubwa nchini Marekani imekataa mahusiano na rapa huyo kwa kusema kuwa “ haivumiliki chuki dhidi ya wayaudi na matamshi yoyote ya chuki”


Ushirikiano wa mkataba unao fahamika kwa jina la didas Yeezy na Mr West ulikuwa ukitazamwa upya baada ya kuonekana kwa fulna  iliyoandikwa "White Lives Matter" katika Wiki ya Mitindo ya Paris.

Siku kadhaa baada ya onesho hilo mwamba  West alichapisha maoni ya chuki dhidi ya Wayahudi kwenye akaunti yake ya Twitter. Ndipo kampuni hiyo ikaamua kufuta mkataba na kueleza kuwa Bidhaa zake zitaondolewa katika soko mara moja, ilisema Adidas.

Kutoka katika jarida maarufu nchini humo Forbes inabaini kuwa Kanye West mpaka sasa atakuwa ameshafirisika kwasababu mikataba hiyo ilikuwa ni sehemu kubwa ya Utajiri wake.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags