Adaiwa kuwa na zaidi ya watoto 500

Adaiwa kuwa na zaidi ya watoto 500

Jonathan Jacob Meijer mwenye umri wa miaka 41 raia wa Uholanzi amepigwa marufuku kusambaza mbegu zake za kiume baada ya kugundulika kuwa na watoto zaidi ya 550 duniani kupitia utoaji wa msaada wa mbegu za kiume za uzazi.

Mwanaume huyo mnamo mwaka 2017 alizuiliwa kutoa mbegu za uzazi kwenye kliniki ya masuala ya uzazi nchini Uholanzi baada ya kufahamika kuwa alikuwa amezalisha watoto zaidi ya 100.

Aidha inaelezwa kuwa badala ya kuacha kuendelea na utoaji wa msaada huo, Jonathan aliendelea kutoa mbegu zake nje ya nchi yake na kwa njia ya mtandao.

Mahakama ya Uholanzi mjini The Hague imemwambia atoe orodha ya kliniki zote alizowatumia na kuziagiza ziharibu mbegu zake.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags