50 Cent mdhamini timu ya wasichana

50 Cent mdhamini timu ya wasichana

‘Rapa’ kutoka nchini Marekani 50 Cent amewashitua wengi baada ya kufanya maamuzi ya kuwa mdhamini wa ‘timu’ ya wasichana wenye umri chini ya miaka 14 ya mpira wa miguu kutoka Wales.

‘Timu’ hiyo ya AFC Rumney ilidhaminiwa na mkali huyo kutokana na mmoja wa mzazi wa mchezaji katika ‘timu’ hiyo kufanya kazi na Cent katika ziara yake ya ‘kimuziki’ kwa siku za hivi karibuni ambapo wazazi walimshawishi aongee na mwanamuziki huyo kuhusu kufadhili ‘timu’ hiyo.

Richie Brown ambaye ni ‘meneja’ wa ‘timu’ hiyo kufuatia taarifa yake ameeleza kuwa wachezaji hao wasiwe na hofu maana 50 Cent amekubali kuwadhamini na kufadhili vifaa vya kuchezea.

Hivyo basi wachezaji watavaa ‘jezi’ za ugenini za tracksuit iliyoandikwa G-Unit ambalo ni kundi la muziki wa hip-hop kutoka Marekani, huku chini kidogo ya track hiyo ikiandikwa jina la 50 Cent.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurukaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags