50 Cent audhihaki muonekano wa Madonna

50 Cent audhihaki muonekano wa Madonna

‘Rapa’ mkongwe kutoka nchini Marekani, #50Cent inadaiwa kuwa ameudhihaki muonekano wa mwanamuziki #Madonna kwa kumcheka baada ya ‘kumposti’ katika ukurasa wake wa Instagram.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari inaelezwa kuwa ‘rapa’ huyo aliingia kwenye mtandao wake wa #Instagram na kuweka picha ya Madonna akiwa amevalia vazi la dhahabu akimfananisha na mdudu mweusi.

Hata hivyo Madonna mpaka sasa hajatoa maoni yoyote kuhusiana na dhihaka hiyo aliyoifanya 50 Cent kwa kitendo cha ‘kupost’ picha yake na kumfananisha na mdudu.

Imekuwa kawaida kwa ‘rapa’ huyo kumkashifu mwanamuziki huyo maarufu wa nyimbo za Pop, mwaka 2022, 50 Cent alifanya hivyo hivyo kwa ‘kuposti’ mitandaoni picha mbaya ya Madonna.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags