50 Cent amshitaki Ex wake kwa kumchafulia CV

50 Cent amshitaki Ex wake kwa kumchafulia CV

‘Rapa’ kutoka Marekani 50 Cent amemshitaki mpenzi wake wa zamani aitwaye Daphne Joy kwa kumshutumu hadharani kuwa aliwahi kumfanyia unyanyasaji wa kimwili.

Kwa mujibu wa tovuti ya Tmz News imeeleza kuwa katika hati zilizowasilishwa Mahakamani siku ya Jumatatu Mei 6, zilieleza kuwa Machi 28, Daphne alichapisha ujumbe kupitia ukurasa wake wa Instagram akimshutumu 50 kumfanyia unyanyasaji huku akidai kuwa haoni kama anafaa kukaa na mtoto wao aitwaye Sire.

Hayo yote yanatokea baada ya ‘rapa’ huyo kutaka haki ya malezi ya mtoto wake kutokana na mzazi mwenziye kuhusishwa katika biashara ya ngono kwenye kesi zinazomkabili mkali wa hip-hop Diddy.

Hata hivyo 50 Cent amedai kuwa shutuma hizo zilizotolewa na Daphne zimeharibu sana sifa yake ya biashara, muziki na kuibuka kwa kesi za mara kwa mara za malezi ya mtoto.

50 Cent na Daphne waliwahi kuwa na mahusiano ambayo yalidumu mwaka mmoja tuu ambapo yalianza rasmi mwaka 2011 na kuachana 2012, wawili hao walibahatika kupata mtoto wa kiume aitwaye Sire.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post