35 wafariki baada ya kutumbukia kwenye kisima

35 wafariki baada ya kutumbukia kwenye kisima

Takriban watu 35 wamefariki dunia baada ya kutumbukia kwenye kisima walipokuwa wakisali katika hekalu moja katika jimbo la kati la India la Madhya Pradesh.

Kisa hicho kilitokea katika hekalu mjini Indore katikati mwa India, huku wengine 18 wameokolewa na mtu mmoja bado hajapatikana katika ajali hiyo.

Inaelezwa kuwa tukio hilo lilitokea siku ya jana Alhamisi wakati wa hafla ya maombi iliyoandaliwa katika hekalu la Beleshwar Mahadev Jhulelal kwenye hafla ya sherehe ya Kihindu ya Ram Navami.

Polisi nchini humo wameeleza kuwa umati mkubwa wa waumini walikuwa wamesimama kwenye slab ya zege iliyofunika kisima ambacho kiliporomoka kwa uzito wao, na kuwatumbukiza watu wengi kwenye kisima chenye kina cha futi 40 (12m).

Taarifa kutoka kwa vyombo vya habari imesema kuwa hekalu hilo lilijengwa baada ya kisima hicho kufukiwa takribani miongo mine iliyopita

Aidha watu 18 walilazwa katika hospitali baada ya kuokolewa na wengine wawili wameruhusiwa kwenda nyumbani, huku waokoaji wakiendelea na jitihada za kumpata ambae amesalia ndani ya kisima

Waziri Mkuu Shivraj Singh Chouhan ametangaza fidia ya rupia 500,000 ($6000; £4900) kwa jamaa wa marehemu na rupia 50,000 kwa waliojeruhiwa.









Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags