21 wafariki baada ya basi kuangukia darajani

21 wafariki baada ya basi kuangukia darajani

Takribani watu 21 wamefariki dunia na wengine 18 kujeruhiwa baada ya basi lililokuwa limebeba watalii kuanguka mita 30 kutokea kwenye daraja na kuwaka moto karibu na jiji la Venice nchini Italia usiku wa kuamkia leo.

Kwa mujibu wa mamlaka basi hilo lililoangukia karibu na njia ya reli katika laini za umeme, lilikuwa limebeba watu wa mataifa mbalimbali wakiwemo na watoto.

Aidha Meya wa Venice Luigi Brugnaro ameizungumzia ajali hiyo na kusema kuwa ni msiba mbaya sana na ameeleza kuwa kwa haraka ameamuru mji huo kuingia kwenye maombolezo kuwakumbuka waliopoteza katika ajali hiyo.

Naye Waziri Mkuu wa nchi hiyo Giorgio Meloni ametoa pole kwa niaba yake na Serikali nzima kwa wote walioathirika katika ajali hiyo iliyotokea Jumanne usiku.

Uchunguzi juu ya chanzo cha ajali hiyo unaendelea huku maafisa wa polisi wakisema upo uwezekano wa kuongezeka kwa idadi ya vifo.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags