Zaidi ya watu 10 wamefariki dunia na wengine 20 wamelazwa hospitalini baada ya basi la harusi kuanguka katika eneo la mvinyo nchini Australia.
Abiria hao walikuwa wakirejea kutoka harusini katika kiwanda cha mvinyo Jumapili usiku ambapo gari hiyo lilipinduka kwenye eneo karibu na Greta huko Hunter Valley, New South Wales. Huku dereva wa basi hilo mwenye umri wa miaka 58 amekamatwa.
Ajali hiyo ilitokea majira ya saa 23:30 za eneo basi lilibingiria lilipokuwa likizunguka kwenye barabara kuu.
Idadi ya waliofariki inaweza kuongezeka, huku abiria 25 wakipelekwa hospitalini wawili kati yao wakisafirishwa kwa ndege kutoka kwenye ajali hiyo, Chapman alisema
Kaimu Kamishna Msaidizi wa Polisi Tracy Chapman alisema wageni walikuwa wakisafiri hadi Singleton "pengine kwa ajili ya malazi yao".
Leave a Reply