‘Royal Tour’ yatajwa kuimarisha biashara ya usafiri wa anga

‘Royal Tour’ yatajwa kuimarisha biashara ya usafiri wa anga

Filamu ilionesha utamaduni na historia ya kipekee ya Tanzania imetajwa kuimarisha biashara ya anga kwa kufanikiwa kusajili ndege 31 ikilinganishwa na 12 zilizosajiliwa mwaka 2022 Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), mwaka 2023 imeeleza.

Hilo lilitokana na kuendelea kuimarika kwa biashara ya usafiri wa anga, maboresho ya viwanja na mitambo ya kuongozea ndege, na juhudi za Serikali katika kukuza utalii kupitia programu maalumu ya 'Tanzania - The Royal Tour'.

Taarifa ya hali ya uchumi wa Taifa kwa mwaka 2023 iliyowasilishwa bungeni leo Juni 13, 2024 inaeleza katika kipindi hicho, mamlaka ilikagua na kutoa vyeti vya ubora kwa ndege 120 ikilinganishwa na ndege 147 mwaka 2022.

“Hadi Desemba 2023, mashirika 25 ya ndege za kimataifa yalitoa huduma kwa utaratibu wa mikataba ya usafiri wa anga baina ya Tanzania na nchi nyingine (Basa) ikilinganishwa na mashirika 23 katika kipindi kama hicho mwaka 2022,” inaeleza taarifa hiyo.

Ongezeko la ndege za kimataifa inaelezwa lilichangiwa na kuendelea kukua kwa soko la usafiri wa anga nchini, hivyo kuvutia mashirika mapya.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mwaka 2023, abiria waliosafiri kwa njia ya anga walikuwa 6,820,541 ikilinganishwa na abiria 5,718,395 mwaka 2022, sawa na ongezeko la asilimia 19.3. Kati ya hao, abiria 3,801,252 walisafiri ndani ya nchi na abiria 3,019,289 walisafiri nje ya nchi.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags