‘Kocha’ wa Geita Gold kikaangoni

‘Kocha’ wa Geita Gold kikaangoni

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji Geita, #ZaharaMichuzi amemtaka ‘kocha’ mkuu wa ‘timu’ ya #GeitaGold, #HemediSuleiman, kufika ofisini kwake kwa lengo la kutolea ufafanuzi juu matokeo mabovu na sababu ya ‘timu’ hiyo kutofanya vizuri.

Akizungumza na vyombo vya habari akiwa mkoani Geita, Zahara amesema haridhishwi na mwenendo wa ‘timu’ hiyo huku akimtaka ‘kocha’ na benchi lake la ufundi wafike kumueleza vikwazo vinavyokwamisha ‘timu’ hiyo kutofanya vizuri.

Aidha mkurugenzi huyo amekiri matokeo ya suluhu waliyoyapata Geita Gold FC ugenini mkoani #Mbeya dhidi ya #TanzaniaPrisons yanatoa mwanga wa mabadiliko lakini lazima hatua thabiti zichukuliwe.

Ikumbukwe kuwa #GeitaGoldFC inafundishwa na ‘kocha’ Hemedi ambaye tangu apewe dhamana hiyo, imecheza michezo nane ya ‘ligi’ kuu ya Tanzania bara na kupoteza michezo minne, kupata sare tatu na ushindi mmoja pekee.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags