‘Calm Down’ ya Rema bado haijaisha makali

‘Calm Down’ ya Rema bado haijaisha makali

Wimbo wa mwanamuziki kutoka nchini Nigeria #Rema ‘Calm Down’ umeweka historia ya kuwa wimbo wa kwanza wa Afrika kuingiza bilioni 1 zinazohitajika nchini Marekani.

Tovuti ya Daily Post News imeeleza kuwa kulingana na kampuni za American Music Stats, Data Chati, ‘Calm Down’ imepata zaidi ya mitiririko bilioni 1 inayohitajika nchini humo.

Mwezi Agosti mwaka jana, ‘Calm Down remix’ aliyoifanya mwanamuziki huyo na #SelenaGomez ilikuwa wimbo wa kwanza Afrika kufikisha alama bilioni 1 katika historia ya Spotify.

Toleo la 'Calm Down' lilitambuliwa na Guinness World Record kama wimbo namba moja kwenye chati ya kwanza ya utiririshaji ya kikanda duniani, (MENA).

Ikumbukwe wimbo huo ambao umeteka mashabiki wengi ulimwenguni nakufanikisha Rema kuzidi kupata umaarufu ndani na njee ya Nigeria ulitoka na kusikika mwaka 2022 na mwaka 2023 remix ya Calm Down iliweza kupata tuzo ya Grammy katika kipengele cha wimbo bora wa Kimataifa.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags