Will Smith atua Tanzania kimya kimya

Will Smith atua Tanzania kimya kimya

Moja ya story inayobamba katika mitandao ya kijamii ni hii ya Msanii wa Filamu kutokea nchini Marekani Will Smith kuja nchini Tanzania kimya kimya.

Unaambiwa kwa mara nyingine tena Tanzania imepata ugeni mzito wa msanii huyo kupitia sekta ya utalii ambapo amekuja na kupata fursa ya kutembelea Mbuga ya Wanyama Serengeti.

Will Smith ametuthibitishia hilo katika ukurasa wake wa Instagram kuwa alikuwa nchini kwa ajili ya kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii iliwemo Mbuga ya Wanyama ya Serengeti.

“Seeing the great migration in person was Wild Welcome to the Serengeti baby,” ameandika Will Smith katika ukurasa wake huo wa Instagram akiambatanisha na video inayomuonesha yupo mbugani.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags