Mkongwe wa ndondi, Mike Tyson yupo kwenye mipango ya kurejea tena ulingoni, licha ya kupoteza pambano lake la mwisho alilocheza Novemba, 15, 2024 dhidi ya Jake Paul.
Utakumbuka kuwa Mike alizichapa kwa mara ya kwanza na kijana huyo mwenye umri wa miaka 28 ikiwa ni baada ya kustaafu ngumi miaka 20 iliyopita. Huku pambano lao likiibua mitazamo mingi hadi kufikia kutazamwa zaidi ya mara milioni 100 Netflix.
Hivyo basi mpango uliopo ni Tyson (58) kupigana na mkongwe mwenzake, Evander Holyfield (62) ambaye alipigana naye mwaka 1996. Ambapo pambano hilo lilimalizika raundi ya 11 baada ya Tyson kumng’ata sikio Evander.
Akizungumza katika onyesho la kwanza la filamu inayofahamika kama 'An American Story' kutoka kwa muigizaji Chuck Zito, Mike alisema baada ya pambano lake la Novemba linafuata jingine lake na Evander Holyfield.
Aidha kwa upande wa Holyfield aliwahi kustaafu ngumi mwaka 2021, kisha alirejea ulingoni kupigana na Mwanamichezo wa Mapigano ya MMA, Vitor Belfort mwenye miaka 47. Pambano hilo lilimalizika kwa Holyfield kula kichapo katika raundi ya kwanza.
Leave a Reply