Fahamu sababu maandishi ya Ambulance kugeuzwa

Fahamu sababu maandishi ya Ambulance kugeuzwa

Watu wengi wamekuwa wakitamka neno ambulance au kuliona gari hilo la kubebea wagonjwa bila ya kugundua siri iliyopo katika uandishi wa neno ambulance, ambalo huandikwa mbele na pembeni ya gari hilo.

 Katika gari hilo la kubebea wagonjwa neno ambulance ambalo mara nyingi huandikwa kwa maadishi mekundu, huwa limegeuzwa yaani nyuma mbele na mbele nyuma, badala ya kuandikwa AMBULANCE limeandikwa ECNALUBMA.

Sababu kubwa ya kugeuza maneno hayo ni kutokana na vioo vya magari vya kutazama nyuma, ili kuona magari mengine huwa ni vioo vya convex. Vioo hivi huwa na tabia ya kubadilisha muonekano yaani upande wa kulia wa kitu huonekana kama upande wa kushoto.

Hivyo basi neno AMBULANCE limeandikwa kinyume kwa makusudi kwa sababu linapo onekana kwenye kioo cha pembeni au cha mbele cha gari lingine, taswira ya neno hilo hugeuka na kusomeka vizuri, hivyo humsaidia dereva kusoma vizuri neno hilo ili aweze kupisha njia ili gari hilo lipite.Ingawa yapo baadhi ya magari ya wagonjwa yameandikwa kwa mfumo wa kawaida lakini lengo kubwa kwa yale yaliyogeuzwa ni kumsaidia dereva kusoma vizuri neno hilo.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post