Fahamu kuhusu ugonjwa wa u.t.i, fangasi sugu na miwasho ukeni

Fahamu kuhusu ugonjwa wa u.t.i, fangasi sugu na miwasho ukeni

Na Shufaa Nassor

Hellow!!! I hope mko well, am here kuelekezana kuhusiana na maswala mazima ya Afya hususani ya wanawake, maana wengi wenu mnanitambua kama Madam hedhi salama, sasa leo katika  mwendelezo wa topic zetu tutazungumzia jambo ambalo kwasasa linatrenda sana kupitia mitandao ya kijamii. Kuhusiana na swala zima la u.t.i, fangasi sugu na miwasho ukeni.

Fangasi ukeni ni maambukizi ya kawaida ya midomo ya uke (vulva) na ugonjwa huu hujulikana pia kama fangasi kwenye sehemu za siri.

Fangasi inasababishwa na jamii ya fungi anaitwa CANDIDA. Seli za fangasi na bacteria wazuri huishi ukeni bila tatizo lolote. Tatizo linakuja endapo ukuaji wa fangasi hawa ukeni watakuwa wengi kushinda wazuri. Basi hapo ndio inapotokea ugonjwa wa fangas na miwasho mingi.

Kandida mara nyingi huwepo katika viwango vidogo mwilini. Hata hivyo, katika baadhi ya visa kuna uwezekano fangasi hawa kuwepo kwa wingi na kusababisha maambukizi.

Huu kwa kawaida sio ugonjwa unaosambazwa, kwa njia ya kujamiina (STI), lakini kwa wakati mwengine unaweza kusambazwa kati ya wapenzi.

Wakati mwingine maambukizi haya yanaweza kujirudia. Yanaweza kutokea kipindi cha msongo wa mawazo, hasaa kwa watu wenye kisukari au magonjwa ya mfumo wa kinga.

DALILI ZA FANGASI

  • Kukojoa mara kwa mara.
  • Mkojo kuwa na harufu kali.
  • Maumivu ya misuli na tumbo hasa chini ya kitovu.
  • Maumivu ya kiuno.
  • Kuwashwa sehemu za siri.
  • Kuhisi maumivu wakati wa kujamiiana au kukojoa.
  • Kupata vidonda vya ukeni.
  • Kuvimba na kuwa mwekundu kwa mdomo wa inje wa uke.
  • Kuhisi kuwaka moto sehemu za siri baada ya tendo la ndoa.
  • Kutokwa na uchafu wa rangi nyeupe au kijivu unaoweza kuwa mwepesi au mzito au majimaji. 

VISABABISHI VYA FANGASI.

  1. Mabadiliko ya homoni katika kipindi cha upevushwaji wa mayai kwa mwanamke kipindi cha ujauzito, utumiwaji wa uzazi, wa mpango na kukoma kwa hedhi.
  2. Upungufu wa kinga mwilini: Mtu mwenye upungufu wa kinga mwilini kama vile mwenye kuugua kansa, ukimwi, magonjwa mbalimbali yenye kupunguza kinga ya mwili.
  3. Kukosa usingizi stress, vidonda sehemu za siri,matumizi ya antibiotics, kuweka marashi sehemu za siri.
  4. Watu wanaougua kisukari ambao hawawezi kudhibiti kwa kutumia dawa za kisukari, inakuwa kwenye damu na hicho kisukari ndiyo chakula kikuu cha hao fangasi.

Hata wanawake ambao wanapenda kula vyakula vya sukari nyingi kama vile chocolates, soda, na vingine vyenye sukari nyingi ambavyo ni chakula cha fangasi.

  1. Mazingira ya joto hii inamaanisha nguo ambazo tunatakiwa kuvaa kama vile chupi za cotton hasa kwa wanawake, hazihitaji joto sababu bacteria wabaya wanakuwa wengi sana na kusababisha miwasho na fangasi.
  2. Kondomu na mbegu za kiume huharibu hali ya asidi iliyopo ukeni ambayo ni ya muhimu sana maana inasaidia kukinga uke usiingiliwe na bacteria wabaya.

MADHARA MAKUBWA YA FANGASI

Kupatwa kwa ugonjwa wa Pelvic Inflammatory Disease (PID) maambukizi katika via za uzazi na kupelekea kuwa mgumba, ndio maana wanawake wengi ni wagumba.

NAMNA YA KUJILINDA NA U.T.I NA FANGASI.

  • Tumia viini lishe na virutubisho i.e food supplements.
  • Kunywa maji mengi angalau glasi nane kwa siku.
  • Epuka matumizi ya pombe na kahawa.
  • Kunywa maji kabla ya kufanya mapenzi na kojoa baada ya kufanya mapenzi.
  • Jitawaze kuanzia mbele kwenda nyuma. (Front to Back)
  • Kata makucha marefu kwa sababu unavyokwenda chooni kujitawaza huwa baadhi ya uchafu unabaki kwenye makucha na ndio chanzo cha wanawake wengi kuwa na U.T.I inayojirudia mara kwa mara.
  • Tumia pads ukiwa kwenye period.
  • Ebuka kujipulizia pafyumu kwenye sehemu za siri.
  • Vaa nguo za ndani za pamba na epuka nguo zilizobana sana.

 

SULUHISHO LA WENGI.

Watu wengi wanapokuwa na U.T.I huenda kupewa antibiotics ambazo huenda kuua bakteria wazuri na matokeo yake baada ya muda U.T.I inarudi kwa kasi sana. 

SULUHISHO LA KUDUMU.

Unapaswa wewe mwanamke usijioshee kila siku badala ya kuweka marashi au sabuni za chemical, zaidi huuwa bacteria wazuri na kuwaacha wale wabaya.

Na pia kutumia dawa bila ushauri kutoka kwa daktari ni hatari kwa afya yako pia kwan kuna wengine wanatumia dawa za kuweka ukeni na baada ya muda ujikuta uchafu unaanza kutoka na mwisho wa siku tatizo uwa kubwa na kupelekea PID.

 

UTAMBUZI WA FANGASI UKENI.

Utambuzi kwa kawaida hufanywa kulingana na dalili na uchunguzi wa kimwili, ikiwa utambuzi haujathibishwa, sampuli ya majimaji ya ukeni huweza kuchukuliwa na kupimwa kwa uwepo wa fangasi. 

MATIBABU YA FANGASI UKENI

Tina ya fangasi ukeni hutegemea kiwango cha maambukizi na dalili alizonazo, matibabu hujumuisha dawa ya fangasi.

Dawa ya kutibu fangasi ukeni huweza kupakwa kama krimu, kwenye midomo ya uke, kuingizwa kama vidonge vya ukeni au kumezwa kma vidongwe.

Ni rahisi kunywa vidonge, lakini krimu na vidonge vya ukeni hupoza mwasho na maumivu ya ngozi. Kwa kawaida hakuna ulazima wa mtu wa mtu kutibiwa ikiwa haonyeshi dalili zozote.

Njia za asili kutibu fangasi ukeni zinaweza kusaidia kuleta nafuu, lakini ni muhimu kukumbuka kuwa baadhi ya njia hizi zinaweza kua na madhara mengine(side effects)

KINGA YA FANGASI UKENI

Jinsi ya kujikinga fangasi ukeni ni pamoja na kudumisha usafi sehemu za siri kwa maji safi, kuepuka kuvaa nguo za ndani zisizoruhusu joto na unyevuunyevu kutoka huweza kusaidia maambukizi haya, hasa katika maeneo yenye hali ya hewa ya unyevuunyevu.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags