Chumba cha faragha alichopewa Mbappe

Chumba cha faragha alichopewa Mbappe

Nyota wa soka wa Ufaransa Kylian Mbappé amepewa chumba cha faragha katika kituo cha mazoezi cha Real Madrid kufuatia uhamisho wake kutoka Paris Saint-Germain.

Jengo hilo lenye thamani ya pauni milioni 100, lililofunguliwa mwaka 2005, halitozi gharama yoyote kwa wachezaji wa Madrid, huku kila mmoja akiwa na chumba chake kikiwa kimelindwa kwa alama za vidole.

Utakumbuka kuwa Jumatatu Juni 3,2024, katika kurasa rasmi za Madrid ambao pia ni mabingwa wa Klabu Bingwa Barani Ulaya kulichapishwa taarifa ya kuidaka saini ya Mbappe.

Aidha nahodha huyo wa Ufaransa amesaini mkataba wa miaka mitano na Real Madrid wenye thamani ya Euro 12.8 milioni kwa mwaka baada ya kodi, ambapo atapokea bonasi ya kusaini zaidi ya Euro 85 milioni kutoka kwa Madrid kwa kipindi tofauti ndani ya huo mkataba wake.

Mbappe (25) aliigharimu PSG pauni milioni 166 mwaka 2018 lakini aliondoka bila malipo baada ya mkataba wake kumalizika.

Endapo PSG ingemuuza staa huyo ingejipatia karibu Pauni 220 milioni (Euro 187.5 milioni) ya gharama ya jumla.

Mbappe ndiye mfungaji wa muda wote wa PSG akifunga mabao 256 katika mechi 308 alizocheza tangu ajiunge na miamba hito ya Ufaransa akitokea AS Monaco.

Pia, staa huyo amewahi kuwa mchezaji bora wa msimu mara tatu katika Ligi ya Ufaransa 2018, 2019 na 2022.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags