Anna Kane achomoa betri kesi ya Diddy

Anna Kane achomoa betri kesi ya Diddy

Mke wa zamani wa nyota wa NHL Evander Kane, Anna Kane ameweka wazi kuwa yeye ni moja ya watu ambao wamewasilisha mashitaka yao kufuatia na kesi zinazomkabili Diddy Combs za unyanyasaji wa kingono.

Anna ameweka wazi kuwa aliwasilisha malalamiko ya unyanyasaji wa kingono Desemba 2023 akijitambulisha kama Jane Deo huku akidai kuwa alinyanyaswa kingono na Diddy na wenzake alipokuwa na umri wa miaka 17 tukio lililotokea mwaka 2003.

Kwa mujibu wa tovuti ya ‘New York Post’ Anna amedai kuwa alipelekwa kwenye Studio ya Diddy ‘House Recording Studio’ iliyopo jijini New York ambapo Combs na wenzake walimtilia madawa kwenye pombe na kumnyanyasa kimwili.

“Nilitaka kuendelea kutumia jina la bandia kufanikisha haki juu ya yaliyotokea nikiwa kijana mdogo, Hata hivyo, jaribio la kunilazimisha kutumia jina langu lilikuwa ni njia ya kunitisha na Sitishiki” alisema kupitia wakili wake.

Kwa sasa Diddy amezuiliwa katika gereza la MDC Brooklyn, Combs alikamatwa na kutupwa gerezani Septemba 16 jijini Ney York kwa makosa makubwa ya unyanyasaji wa ngono, usafirishaji haramu wa watu huku kesi yake ikianza kusikilizwa Me 5, 2025.

Anna na Evander Kane walifunga ndoa mwaka 2018 na walipata mtoto mmoja wa kike, wawili hao walitalikiana mwaka 2021 baada ya Anna kumtuhumu Evander kuwa mraibu wa Kamari.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags