Alama za vidole vya Tupac na Biggie zaingizwa sokoni

Alama za vidole vya Tupac na Biggie zaingizwa sokoni

Kadi zenye alama ya vidole vya waliokuwa wasanii wa muziki wa hip-hop marehemu Tupac na Biggie walizosaini baada ya kukamatwa kwao zaingizwa sokono.


Alama hizo zinauzwa na Wafanyabiashara Wakuu wa Kumbukumbu za Kitaifa kwenye mtandao wa Momentintime.com, kwa gharama ya dola 225,000 kwa kila moja ambazo ni zaidi ya tsh 564.4 milioni.


Kadi yenye alama za vidole vya Tupac ilitokana na kukamatwa kwake mwaka 1995 kutokana na kupatikana na hatia ya unyanyasaji wa kingono na kumpiga shabiki wa kike anayeitwa Ayanna Jackson jambo lililopelekea ahukumiwe jela kifungo cha mwaka mmoja na miezi mitano lakini alitumikia kifungo hicho kwa miezi 9.



Aidha kwa upande wa Biggie kadi hiyo ni ya mwaka 1995 kwa kesi yake ya wizi na shtaka la unyanyasaji aliofanya Pennsylvania hata hivyo mashtaka ya wizi yalitupiliwa mbali baadaye.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post