Bonge La Dada: Nafanya Shoo Nyingi Zaidi Ya Mbosso

Bonge La Dada: Nafanya Shoo Nyingi Zaidi Ya Mbosso

Densa na video vixen maarufu nchini, Queen Fraison 'Bonge la Dada' amefunguka kupokea jumbe mbalimbali kutoka kwa mashabiki zikidai amepotea kwenye gemu ndani ya muda mfupi.

Akizungumza na Mwananchiscoop, Bonge la Dada amesema maneno ya mashabiki mtandaoni hayampi shida kwa sababu kila anachokifanya anaona yupo sahihi.

"Maneno ya watu mtandaoni hayanipi shida kwa sababu siwezi mpangia na kumzuia mtu cha kuongea kila mtu anamtazamo wake na namna anavyotaka yeye kuongea.

“Kwa hiyo wakisema nacheza style moja mimi nacheza iliyotambulika kwenye wimbo na wakisema nimeanza kuchuja ni wao. Lakini ninachofanya naona kipo sahihi," amesema Bonge la Dada.

Amesema licha ya maneno hayo mitandaoni, bado anaendelea kupokea shoo nyingi, lakini haimzuii kutekeleza majukumu ya kupafomu kwenye shoo za boss wake Mbosso ambaye walianza kufanya kazi tangu 2020.

"Nilianza safari ya kucheza 2019 lakini kufanya kazi na Mbosso nilianza mwaka 2020. Kwenye suala la shoo ni nyingi lakini wingi wake hainizuii kufanya kazi na boss naweza nikaenda kwenye shoo zangu lakini nikahudhuria pia kazi zake.

“Muda ambao nimemaliza shoo zangu huohuo naweza nikaondoka nikarudi kwenye shoo ya boss. Maana imewahi kutokea sio mara moja au mbili nipo mkoa mwingine kwenye shoo yangu nikabadili tiketi nakurudi kufanya shoo ," amesema Bonge la Dada.

Amesema kitu pekee ambacho kinamtofautisha na madensa wengine ni muonekano na namna alivyotofauti kwenye uchezaji wake.
"Kuimba ni kipaji, kama ikitokea nikiweza nitaimba kama nitaweza lakini kama sitoweza sitoimba. Kwa sababu sio kitu ambacho kilikuwa chalazima kwangu lakini ni suala linalohitaji muda sana kwangu," amesema Bonge la Dada.

Aidha, Bonge la Dada amesema kazi ya udensa sio uhuni kama wengi wanavyodhania bali ni kazi kama kazi nyingine na kwa yeyote anayehisi ana kipaji hicho asikipoteze.
" Kama unavyojua sanaa inatakiwa uwe tofauti, mbunifu, na muonekano ambao mtu akikuangalia anashawishika aendelee kukuangalia. Kwa hiyo kwa wanaosema sanaa ni uhuni wasijipotoshe, " amesema Bonge la Dada.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags