Kwa mujibu wa jarida maarufu la fashion na mitindo Marekani 'Complex Style' limemtaja Asap Rock kama rapa ambaye ameongoza kwa kuvaa vizuri mwaka 2024.
Rock ambaye pia ni Baby Dady wa mwanamuziki Rihanna, ametangazwa kuwa rapa namba moja kwenye kuvaa na mitindo ya mavazi huku akifuatiwa na Lil Yachty, Kendric Lamar, Tyler The Creator, Playboi Carti, Card B, Doja Cat, Smino, Tierra Whack na Travis Scott.
Desemba 3,2024 Asap Rocky alishinda Tuzo ya Mvumbuzi wa Utamaduni kwenye tuzo za British Fashion Awards 2024, tuzo ambayo hupewa mvumbuzi na mtengenezaji wa picha za fashion anayeongoza katika tasnia ya burudani.
Mbali na kufanya vizuri kwenye muziki Rocky amekuwa na athari kubwa kwenye tasnia ya ubunifu, fashion na mitindo maarufu mwaka huu.
Leave a Reply